Thursday, 4 June 2015

mrembo matata afariki dunia akiwa anaongeza makalio huko marekeni. soma hii ni muhimu sana kwa wanawake wote.

 Alitamani kuwa na makalio makubwa, baada ya kuchomwa sindano matokeo ilikuwa ni stori nyingine !!
Syringe
Ishu ya wasichana na wanawake kupenda kuongeza maumbile ya miili yao limekua kama ishu ambayo imechukua sana nafasi sehemu mbalimbali duniani.
Tunashuhudia watu wengi wakiongeza makalio kwa kusudi la kuwa wenye mvuto zaidi, na kumekuwepo na vidonge na sasa kuna sindano za kuongeza makalio.
Mahyew
Kelly Mayhew
Leo nimekutana na stori iliyotokea Los Angeles Marekani, ambako msichana Kelly Mayhew mwenye miaka 34 amefariki baada ya kufikishwa St.John’s Espiscopal Hospital, muda mfupi baada ya kuchomwa sindano ya kuongeza makalio.






Kelly Mayhew  Photo via Facebook



Kelly Mayhew  Photo via Facebook
Kelly Mayhew na mama yake walisafiri kutoka Maryland kwenda Rockaway, walikokua wameelekezwa na rafiki yake Kelly ili kwenda kuchoma sindano hiyo ambayo ilikua inatolewa kinyume na utaratibu… mtoaji wa huduma hiyo alijiita daktari lakini hakuwa amesajiliwa na alikuwa hatambuliki kisheria.
Baada ya kuchomwa sindano hiyo, Kelly alianza kupumua kwa shida, akawa anajitupa ovyo chini huku akiishiwa pumzi… baada ya kuhangaika kwa kama dakika ishirini hivi, Kelly alifariki akiwa kwenye mikono ya mama yake.. mpaka Polisi wanafika eneo hilo Daktari alikuwa tayari kashakimbia.



No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...