Tuesday, 12 April 2016

majonzi: Mchezaji wa Uingereza auawa nchini Trinidad


Image caption Adrian St John
Mchezaji chipukizi wa Kriketi raia wa Uingereza amefariki baada ya kuripotiwa kupigwa risasi na majambazi nchini Trinidad.
Adrian St John , mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikichezea chuo cha mafunzo cha Chris Gayle mjini London anaaminika kufariki siku ya Jumapili.
Mchezaji wa kriketi wa West Indies Gayle alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akisema " Ni habari mbaya kusikia ,Rambirambi zangu kwa familia na marafiki." Adrian St. John alikuwa nahodha katika chuo hicho.

Image caption Aliuwa baada ya kusimamisha gari lake ili kuwachukuwa rafiki zake alipovamiwa na kupigwa risasi
Ofisi ya maswala ya mambo ya nchi za kigeni imesema walikuwa kwney mazugumzo na maafisa nchini Trinidad kufuatia kifo cha raia huyo wa Uingereza.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba Bwana St.John, alivamiwa baada ya kusimamisha gari lake ili kuwachukuwa rafiki zake alipovamiwa na kupigwa risasi.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...