Miaka miwili iyopita wiki kama hii , wasichana 267 walitekwa nyara kutoka shuleni kwao na wanamgambo wa Boko Haram .
Suala
lililolaaniwa vikali kimataifa na kuchochea kampeni ya mitandao ya
kijamii iliyojulikana kama #bringbackourgirls na kuweka wazi udhalimu
unaotekelezwa na makundi ya uasi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.Katika ripoti hii maalum mwandishi wa BBC Martin Patience alisafiri hadi Chibok kuongea na familia za wasichana na kutembelea shule ambako walitekwa nyara.
TaswiraKile kinachoonekana kama msikiti unaonekana kupigwa risasi kila mahali , Paa lake limeng'olewa ,
Hiki kilikuwa ni kijiji ambacho huenda kilikua ni makaazi ya makumi kadhaa familia , lakini kwa sasa hakuna mtu anayeishi hapa na vichaka vimemea tena kijijini hapa
Msitu hapa ni mkubwa .. na ni rahisi sana kwa wanamgambo wa Boko Haram kuvamia msafara wowote wa magari ya kijeshi
CHIBOKLakini wakati huo Boko Haram walipokuja kuwateka mamia ya wasichana wa eneo hili walibaki na kumbukumbu za kutisha za usiku huo …..
Wazazi hapa wamebakia kusubiri majibu ya wapi waliko watoto wao.
Miongoni mwao ni Mariam Abubakar.
Mwanaye Han Satu alikua na umri wa miaka 17 alipotekwa … alipenda mitindo
''Muda mfupi tu kabla ya kuchukuliwa alikua ameniomba nimnunulie mashine ya kushona nguo''alisema Myrama Abubakar.
Mbele ya nyumba yake ya matope Maryama alivuta nguo alizoacha binti yake .
Alichukua vazi alilolipenda na kuliweka kwenye magoti yake .
Lakini mitihani haikufanyika . Nitaitunza gauni hii mpaka atakaporudi alisema mzazi huyo.
Na baade nilizungumza na Binta AbuBakar mama yake Maryam ambaye sasa angekua na miaka 19 -
Naomba binti yangu arejee akiwa hai . Lakini kama haitakua hivyo natumai roho yake italala kwa amani . Natumai kumbu kumbu za kutisha alizoziona wakati alipotekwa yatakua ndio mateso yake ya mwisho ,alisema bi AbuBakar.
Maisha yanaendelea kurejea taratibu katika hali ya kawaida mjini Chibok na usalama unaimarika.
Lakini inawezekanaje katika dunia ya sasa kwamba hakuna msichana hata mmoja alieweza kuokolewa?
No comments:
Post a Comment