![]() |
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino |
Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shirikisho hili litamuunga mkono rais wa sasa wa FIFA GIANNI INFANTINO katika uchaguzi wa FIFA utakaofanyika mwakani.
CAF imeweka hadharani maamuzi hayo katika mkutano wake mkuu uliofanyika nchini MISRI ambapo AHMAD amesema wao kama shirikisho na kwaniaba ya vyama vya soka vinavyounda shirikisho hilo watampigiua kura INFANTINO,
![]() |
Rais wa CAF Ahmad Ahmad |
Rais wa shirikisho la soka nchini MOROCCO FOUZI LEKJAA amesema mbali na kumpigia kura INFANTINO watazunguka naye sehemu yoyote dunian kama sehemu ya kampeni ili kutangaza yale mema aliyoyafanya tangu aingie madarakani.
Kwa mujibu wa tariifa mbalimbali, sera ya INFANTINO ya kuongeza nafasi za idadi ya mataifa ya afrika yatakayoshiriki katika fainali za kombe la FIFA la dunia pamoja na ahadi zinazotekelezeka ndiyo sababau kubwa iliyopekea CAF kutangaza kumuunga mkono katika uchaguzi ujao.
![]() |
Rais wa FIFA Gianni Infantino |
Mwezi june mwaka huu Infantino alitangaza kuwa atawania tena nafasi hiyo ya juu kabisa katika mamlaka ya soka duniani katika uchaguzi utakaofanyika mwezi JUNE mwakani jijini PARIS ingawa mpaka hivi sasa hakuna mtu aliyejitokeza kutaka kupambana naye katika nafasi hiyo ya URAIS.