Wednesday, 28 May 2014

eo ni Kumbukumbu ya mwaka 1 toka Albert Mangwea afariki.

Ngwea
Ilikua ni mchana May 28 2013 ndipo zilipotoka taarifa ambazo kulingana na ukubwa wa jina la mangwea Tanzania hakuna aliyekua tayari kuamini kama ni kweli Mangwea kafariki dunia,zilianza taratibu za kuthibitisha taarifa hizi ambapo baadae ilithibitika kweli Mangwea amefariki dunia.
Mpaka sasa ripoti kutoka hospitali ya South Africa familia haijawa tayari kuiweka wazi,kutoka Morogoro nimepata taarifa kuwa leo kutakuwa na ibada asubuhi kisha jioni kutakua na tamasha la kumkumbuka Mangwea ambapo itakua ni kumchangia mama yake Mangwea na imeandaliwa na baadhi ya wadau wa Morogoro na kupata baraka toka kwa Familia ya Mangwea.

Wachezaji 2 wa Ujerumani wapata ajali nchini italy.

Wachezaji 2 wa Ujerumani katika ajali


Wachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia
Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Ujerumani itakayoshiriki kombe la dunia hukop Brazil mwezi ujao
wamenusurika baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakiwa Italia.
Benedikt Hoewedes na Julian Draxler walikuwa ndani ya magari tofauti katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya magari ya Mercedes .
Moja ya magari yaliyohusika iliwagonga wapita njia wawili karibu na makahawa wanakoiswahi timu ya taifa ya Ujerumani.
Mwathiriwa moja anauguza majeraha mabaya .

Wachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia
Ajali ya pili ilimhusisha dereva wa mbio za magari ya langalanga wa Mercedes , Nico Rosberg.
Hoewedes na Draxler ni wachezaji wa timu ya Schalke 04 walioitwa katika timu ya taifa.
Wenyeji wao kampuni ya Mercedes-Benz imetoa taarifa kusema kuwa itashirikiana na maafisa wa polisi kutathmini kilichotokea .
Timu hiyo ya Ujerumani inatarajiwa kuendelea na kambi ya mazoezi katika mji wa Tyrol Kusini mwa Italia hadi juni mosi. .

Tuesday, 27 May 2014

MAFURIKO YAITIKISA CHINA , ZAIDI YA  20 WAFARIKI DUNIA .

Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.30 AMNi dhoruba kali iliyoleta majonzi Kaskazini mwa China ambako mpaka sasa tayari watu 26 wamefariki na wengine 10 hawajulikani walipo huku vyombo vya usalama na uokoaji vikizidi kutafuta njia ya kuepusha maafa zaidi kutokana na hali ya hewa.
Kwenye eneo la Guangdong ni watu 15 wamefariki toka Jumatano iliyopita na wengine watano hawajulikani walipo kutokana na maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha.
Picha zote hizi unazoziona zimepigwa May 25 2014 ambapo hii inaonyesha moja ya familia kwenye eneo hilo ikipata chakula juu ya maji yaliyojaa nyumbani kwao
Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.22 AM
Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.10 AM
Screen Shot 2014-05-27 at 2.30.01 AMcredits to millardayo 

 bongo movie wapat pigo jingine pata 

Screen Shot 2014-05-27 at 8.56.46 AMTukiwa na wiki moja toka tumzike muongozaji na muigizaji Adam Kuambiana leo asubuhi imetoka taarifa nyingine ya kifo cha miongoni mwa waigizaji wa kike toka Bongo Movie.
Aliefariki ni mwigizaji anaitwa Rachel Haule ambaye kacheza movie mbalimbali ikiwemo Vanesa in Dilema.
Screen Shot 2014-05-27 at 8.56.59 AMChanzo cha kifo chake chake bado hakijafahamika ingawa taarifa za mwanzo zinasema alikua mjamzito na alikwenda Muhimbili kwa ajili ya kujifungua baadae alifanikiwa kujifungua lakini kwa bahati mbaya mtoto alifariki nae hali ilibadilika akapelekwa ICU lakini baadae akafariki.

Monday, 26 May 2014


Video: Tazama wimbo ulioimbwa na wachezaji wa Real Madrid kusherehekea ubingwa wa ulaya


article-2639147-1E35F0C300000578-684_634x423Baada ya kushinda taji la 10 la kihistoria la ligi ya mabingwa wa ulaya, timu nzima ya Real Madrid iliingia studio kuimba wa #HalaMadrid. Wimbo huo tayari umetoka utazame hapo chini……

Video: Tazama wimbo ulioimbwa na wachezaji wa Real Madrid kusherehekea ubingwa wa ulaya

article-2639147-1E35F0C300000578-684_634x423Baada ya kushinda taji la 10 la kihistoria la ligi ya mabingwa wa ulaya, timu nzima ya Real Madrid iliingia studio kuimba wa #HalaMadrid. Wimbo huo tayari umetoka utazame hapo chini……





Raia wenye hasira wawashambulia Bey na Jay Z kwa kuikacha harusi ya Kanye.t.



Kanye-West-famous-friendss
Hii ishu inaonekana kuwa imewagusa watu wengi sio Kim na Kanye peke yake kwasababu mashabiki wenye hasira hivi sasa wameamua kutowaacha hivi hivi na kuwashambulia wanandoa Queen Beyonce na mumewe Jay Z kwa kutofika katika harusi ya Kim Kardashian na Kanye West mjini Florence Italia.
Kupitia mitandao ya kijamii “fans” hao hawakubaki nyuma kuandika wanachojisikia juu ya kitendo hicho ambacho wamesema si uungwana kwa Jay Z kumfanyia hivyo mshkaji wake wa kitambo ambaye ni kama familia kwake kwani sio kweli kwamba yuko juu zaidi yake.
Fans
Awali taarifa zilisambaa na kudai kuwa Jay Z hawezi kuhudhuria harusi ya Kanye kwasababu itarekodiwa na kurushwa katika kipindi cha Keeping up with the Kardashians lakini baadae Info nyingine zikaja kuwa atakuwepo kwenye harusi hiyo kama msimamizi lakini mwisho wa siku hakufika kabisa.


Haya hapa magoli yote 17 aliyoyafunga Cristiano Ronaldo ulaya – yaangalie hapa


article-2639065-1E35B8DA00000578-674_634x465Cristiano Ronaldo ameibuka mfungaji bora wa michuano ya mabingwa wa ulaya kwa mara ya pili mfululizo, msimu huu na msimu uliopita.
Nahodha huyo wa Ureno amefunga magoli 17 msimu huu, hii ni rekodi mpya ya mabao kwenye michuano ya ulaya, akiwa amevunja rekodi ya Messi aliyefunga mabao 15 msimu wa 2011/13.
Unaweza kuyatazama magoli yote hapa…..


Unaambiwa taarifa mpya kuhusu ile ndege ya Malaysia iliyopotea kutolewa kesho.


ndege
Taarifa ya picha kamili za Satelite kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea MH370 zitatolewa kesho kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Kaimu waziri wa usafirishaji wa Malaysia Hishammuddin Hussein ametoa taarifa kuhusu kutolewa data za ndege hiyo wakati akiwa anatembelea kampuni iliyopo katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
ndege2
Familia na ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo iliyopotea mwezi Machi mwaka huu ikiwa imebeba watu 239 katika eneo Kusini mwa Asia wamekuwa wakidai data za ajali hiyo kuwekwa hadharani.
Hatma ya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo bado imebaki kuwa moja ya kitendawili kikubwa kuwahi kutokea katika nyakati za sasa.
Kampuni ya Inmarsat, ambayo Satelite yake ilikuwa ikiwasiliana na ndege hiyo iliyopotea katika dakika za mwisho imesema kuwa haikupewa kibali na mamlaka za Malaysia kuachia taarifa hizo hadharani.
ndege3
Lakini sasa kampuni hiyo na serikali ya Malasysia wanasema wanajaribu kufanya taarifa hizo zitolewe hadharani.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

Unaambiwa taarifa mpya kuhusu ile ndege ya Malaysia iliyopotea kutolewa kesho.

ndege
Taarifa ya picha kamili za Satelite kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea MH370 zitatolewa kesho kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Kaimu waziri wa usafirishaji wa Malaysia Hishammuddin Hussein ametoa taarifa kuhusu kutolewa data za ndege hiyo wakati akiwa anatembelea kampuni iliyopo katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
ndege2
Familia na ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo iliyopotea mwezi Machi mwaka huu ikiwa imebeba watu 239 katika eneo Kusini mwa Asia wamekuwa wakidai data za ajali hiyo kuwekwa hadharani.
Hatma ya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo bado imebaki kuwa moja ya kitendawili kikubwa kuwahi kutokea katika nyakati za sasa.
Kampuni ya Inmarsat, ambayo Satelite yake ilikuwa ikiwasiliana na ndege hiyo iliyopotea katika dakika za mwisho imesema kuwa haikupewa kibali na mamlaka za Malaysia kuachia taarifa hizo hadharani.
ndege3
Lakini sasa kampuni hiyo na serikali ya Malasysia wanasema wanajaribu kufanya taarifa hizo zitolewe hadharani.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

Sunday, 25 May 2014


  • Licha ya urafiki mkubwa walionao, Wanandoa Jay Z na Beyonce waipotezea harusi ya mshkaji wao Kanye West


gauni2gauni1
Hatimaye Rapa maarufu wa muziki wa nchini Marekani Kanye West na mwanadada anayemake headlines kila kukicha Kim Kardashian wamefunga pingu za maisha na kuwa mume na mke huko Florence nchini Italia. Wapenzi hao walisafiri kwa nyakati tofauti kutoka jijini Paris nchini Ufaransa ambako waliungana na familia zao katika ile Pre Wedding Party.
Taarifa zinadai kuwa wanandoa hao wapya walipanga kufunga ndoa hiyo huko Chateau de Versailles lakini sheria za Ufaransa hazikuwaruhusu kufanya hivyo kutokana na hata mmoja wao kutokuwa na uraia wa nchi hiyo.
Cha kushangaza ni kwamba si Jay Z wala Mke wake Beyonce aliyehudhuria katika harusi hiyo na kuishia kutuma salamu za pongezi licha ya kuwepo kwa uvumi kuwa Jay Z atakuwa msimamizi wake kutokana na ukaribu na urafiki mkubwa waliokuwa nao.
Tukio hilo kubwa limehudhuriwa na wageni mbalimbali na watu mashuhuri akiwemo mwanamuziki John Legend na mkewe Chrissy Teigen na muongozaji wa filamu ya 12 Years a Slave Steve McQueen.
Story nyingine kubwa ni kwamba mabosi wa kampuni ya Adidas pia walichagua siku hiyo ya harusi kuzindua tangazo lao la kombe la dunia kwa mwaka 2014 linalomhusisha rapa Kanye West pamoja na mastaa wakubwa wa soka duniani Lionel Messi na Dani Alves.
harusi1harusi2harusi3harusi5

RAY C AMUOKOA kumuokoa Video Queen.



Ray C kumuokoa Video Queen aliyetumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya, Picha na maelezo yake viko hapas


Ray CUnaikumbuka nyimbo ya Ice Cream iliyoimbwa na Noorah? Ni nyimbo nzuri iliyotamba miaka iliyopita na kuvuma zaidi baada ya video yake kutoka ambapo ndani yake kulikuwa na Video queen aliyefahamika kwa jina la Doreen.
Taarifa zilianza kusambaa kuwa mwanadada huyo kwa sasa ametumbukia katika tatizo la matumizi ya dawa za kulevya huku akihitaji msaada mkubwa.
Kupita ukurasa wa Instagram mwanamuziki Ray C ambaye nae aliwahi kukumbwa na tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai kuwa amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya.
Ray C ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram dakika chache zilizopita kuwa ”rayc1982 Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasis yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za madawa ya kulevya,nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine!!roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!!namshukuru Mungu Asubuhi ya juzi Nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen kichwa cha habari Kikiwa Msaada,nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply Mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee,nikampigia akaniambia doren Hali yake si Nzuri kutokana na drugs,moyoni nikawa Nafikiria Huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!!ikawa Kama bahati,tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha madawa Mwananyamala!nilipomuona Doren Kwa Mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo,ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza Tiba ya methadone isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu Nimechoka Maisha ya utumwa nisaidie!!hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambia Kwa uwezo wa Mungu Shetani ameshindwa!!!!!!am soooo happy Doren ameanza Tiba ya methadone!!!wapenzi wote wa bongo flava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye Tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa amani bila utumwa wa shetani.God We Trust!!!I love You my lil sister…..Nawahamasisha wengine huko Mliko mwenye ndugu,Jamaa au rafiki,njoo Katika taasis yetu uweze kusaidiwa!usikubali Maisha ya utumwa wa madawa ya kulevya,njoo tukusaidie…Ray C Foundation pamoja na Kitengo cha Methadone We love you guys,We can help you….”

DIAMOND PLATINUMZ AENDELEA KUONGOZA TUZO  MTV , WATANZANIA TUMUOMBEE JAMAN KWA SABABU ANAUONESHA MZIKI WA KITANZANIA DUNIANI

1
Add a comment...

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...