Monday, 22 February 2016

Kizza Besigye kukamatwa leo,rais mstaafu Obasanjo amesema Uganda haipaswi kuzuia upinzani,

Image captionUganda haipaswi kuzuia upinzani, Obasanjo
Aliyekuwa rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ametaka pande zote pinzani katika uchaguzi wa Uganda kujiepusha na matamshi ya uhasama.
Obasanjo ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya madola uliokuwa ukiangalia vigezo vya kidemokrasia katika uchaguzi uliokamilika nchini Uganda amewashauri viongozi wa uganda kujiepusha na makabiliano na migongano baina yao.
Obasanjo alisema''Uhuru wa kujieleza kutengamana na kuwasilana na umma wa kila kiongozi sharti ulindwe na kama kuna vizuizi dhidi ya kiongozi yeyote lazima iondolewe mara moja''
Image captionUganda haifai kuwazuia viongozi wa upinzani ,Obasanjo
Obasanjo aliyasema hayo bila ya kumtaja kiongozi wa upinzani Kizza Bisigye ambaye kwa sasa amezuiliwa nyumbani kwake.
Aliongezea kuwa ''dosari zilizoshuhudiwa katika uchanguzi mkuu umekuwa na madhara mabaya kwa matokeo ya ukweli haki na uwazi wa uchaguzi huo'' , lakini amesisitiza tofauti kati ya utawala na upinzani zinahitajika kusuluhiswa kupitia mazugumzo.''
Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda alikamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.
Image captionKiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda alikamatwa
Amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo.
Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake.
Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais

Thursday, 18 February 2016

exclusive: video mpya ya nyimbo ya mirror -naogopa ft baraka da prince.official video

wema sepetu : hiki ndicho alichokisema jana baada ya mimba yake kuharibika. inahuzunisha sana.

tazama hapa matokeo yote ya kidato cha nne 2015/16 yaliyotoka hivi punde leo.

on
Baraza la mitiani Tanzania NECTA limetangaza Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 , ambapo  ufaulu  unaelezwa kushuka  kwa 1.85%  toka  69.75%  mwaka 2014  hadi 67.91%  mwaka  2015.Matokeo yote unaweza kuyatazama >>HAPA

Watu 28 wauawa katika mlipuko Uturuki,soma tazama picha za tukio

ShambulioImage copyrightEPA
Image captionHakuna kundi lililodai kuhusika
Watu zaidi ya 28 wamefariki baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara Jumatano jioni, maafisa wa Uturuki wamesema.
Watu 61 wamejeruhiwa.
Gar lililojaa vilipuzi lililipuliwa mabasi ya jeshi yalipokuwa yakipita, kwa mujibu wa afisi ya gavana wa Ankara.
Mlipuko huo ulitokea karibu na Bunge na makao makuu ya jeshi ya Uturuki.
Naibu waziri mkuu Bekir Bozdag amesema hicho ni “kitendo cha ugaidi”.
ShambulioImage copyrightGetty
Image captionMlipuko huo ulisikika kote mjini
Moshi ulitanda angani kutoka eneo hilo na watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mlipuko huo ulisikika kote katika mji huo.
Baadhi ya waliofariki na kujeruhiwa walikuwa raia.
Hakuna kundi lililodai kuhusika kufikia sasa

Tuesday, 16 February 2016

valentine`s day Mbunge Zimbabwe avunja rekodi ya kulana mate na mkewe Afrika.

Image captionMbunge Joseph Chinotimba Zimbabwe
Mbunge mmoja nchini Zimbabwe Joseph Chinotimba ameingia katika kumbukumbu za Afrika baada ya kumbusu mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kunakiliwa barani Afrika.
Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hilo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.
Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa ''Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi barani Afrika''
Image captionBwana Chinotimba na mkewe Vimbai
Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.
Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.

Al-Shabab wavamia kambi ya jeshi Somalia, tazama picha za tukio hapa

Image captionWapiganaji wa al-shabab
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la al-Shabab wamevamia vituo vya polisi pamoja na kambi ya wanajeshi karibu na mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Mji wa Afgoye ulionekana kuwa eneo salama, japo wapiganaji hao walivamia nyakati za usiku na kuua watu kumi, wengi wao wakiwa wanajeshi wa asili ya kisomali.
Wapiganaji hao wa al Shabab walichukua silaha kali na magari ya kijeshi.
Wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanasaidi wanajeshi wa Somalia kulinda taifa hilo, japo mashambulizi ya hivi karibuni yamedhoofisha usalama nchini humo.

Saturday, 13 February 2016

exclusive: video mpya ya diamond platnumz na AKA wa S.Africa, tazama na pakua mzigo mpya hapa

exclusive: video mpya ya diamond platnumz na AKA wa S.Africa, tazam na pakua mzigo mpya hapa

taharuki: Al-Shabab wasema ndio walioshambulia ndege.tazama picha hapa za hiyo ndege

  • Saa moja iliyopita
NdegeImage copyrightHarun Maruf
Image captionNdege hiyo ilitoboka shimo ikiwa angani
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabab kutoka Somalia limesema ndilo lililoshambulia ndege iliyotoboka shimo ikiwa angani mapema mwezi huu.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa barua pepe al-Shabab wamesema shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi operesheni za kijasusi zinazoendeshwa na mataifa ya Magharibi nchini Somalia.
Shimo hilo kwenye ndege hiyo lilitoboka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka Mogadishu, ikiwa futi 10,000 (3,048m) juu angani.
Ndege hiyo ilifanikiwa kutua kwa dharura.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Daallo, iliyokuwa ikielekea Djibouti, ilikuwa imebeba watu karibu 60.
Maafisa nchini Somalia baadaye walitoa video inayoonesha watu wawiliwakimkabidhi abiria mmoja anayeshukiwa kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga kitu kinachoonekana kama Laptop kabla ya mlipuaji kuabiri ndege hiyo.
Msemaji wa serikali anasema kuwa watu hao ndio washukiwa wakuu katika ulipuaji huo.
Inasadikika kuwa mmoja kati ya watu walioleta kipakatilishi hicho alikuwa ni mfanyikazi wa shirika linalohudumu katika uwanja huo wa ndege wa Mogadishu.
Watu 20 wamekamatwa wakiwemo wale wawili walionaswa kwenye video hiyo.

Friday, 12 February 2016

furaha: willium Ruto apata ushindi muhimu mahakama ya ICC

RutoImage copyrightAFP
Image captionBw Ruto amekanusha mashtaka yanayomkabili ICC
Naibu Rais wa Kenya William Ruto amepata ushindi muhimu kwenye kesi yake inayosikizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) baada ya majaji wa rufaa kukubali rufaa yake ya kupinga kutumiwa kwa ushahidi wa mashahidi waliojiondoa.
Hii ina maana kwamba ushahidi ulioandikishwa awali na upande wa mashtaka hauwezi kutumiwa dhidi ya Bw Ruto na mwanahabari Joshua Sang.
Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa upande wa mashtaka unaoongozwa na Fatou Bensouda.
Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita waliokuwa wanahusisha Bw Ruto na ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-08, vilivyosababisha vifo vya watu 1,200, walioondoa ushahidi wao.
Upande wa mashtaka unasema walitishiwa au wakahongwa.
Majaji wa rufaa wamebatilisha uamuzi wa awali wa majaji uliosema upande wa mashtaka unaweza kutumia ushahidi uliowasilisha na mashahidi hao kabla yao kubadili nia.
"Ushahidi ulioandikisha awali uliwasilishwa bila washtakiwa kupewa fursa ya kuwahoji na kuwauliza maswali mashahidi hao,” amesema jaji wa mahakama ya rufaa Piotr Hofmanski.
Bw Sang amefurahia uamuzi huo na kusema maombi yake yamejibiwa.

INNOSAM.BLOGSPOT.COM: video:ommy dimpoz na mchumba wake waki kiss hadhar...

kinasaonlinemedia

INNOSAM.BLOGSPOT.COM: video:ommy dimpoz na mchumba wake waki kiss hadhar...

INNOSAM.BLOGSPOT.COM: video:ommy dimpoz na mchumba wake waki kiss hadhar...

Thursday, 11 February 2016

video:ommy dimpoz na mchumba wake waki kiss hadharani na akiongelea kuitwa shoga na ney wa mitego

video:mahojiano ya baba diamond na sud brown wa clouds fm akiongelea mambo ya familia yake.

hivi punde Watu zaidi ya 56 wafariki huko nchini Nigeria.

Image copyrightAP
Maafisa wa magharibi mwa Nigeria wanasema watu zaidi ya hamsini wameuwawa katika shambulio lililotokea katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika jimbo la Borno.Wanawake wawili walirusha bomu ,na watatu alikamatwa na polisi,hukuakikana kuhusika katika shambulio hilo kwa kudai kuwa wazazi wake wako kwenye kambi hiyo hivyo haiwezekani kwa yeye kufanya kitendo hicho
Zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kuyakimbia makaazi yao kutokana na mashambulio ya kushtukiza katika kipindi cha miaka sita iliyopita kulikosababisha na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

video:mahojiano ya baba diamond na sud brown wa clouds tv akiongelea mambo ya familia yake.

Wednesday, 10 February 2016

Mtanzania auawa kwenye kasino Nairobi nchini kenya

Kilimanjaro
Image captionMtanzania huyo alitoka mkoa wa Kilimanjaro
Raia wa Tanzania ameuawa na umati mjini Nairobi baada yake kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari.
Alijaribu kumsihi msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani simu yake lakini akakatazwa kwa msingi kuwa haikuwa imefikisha thamani ya kuwekwa rehani, walioshuhudia wanasema.
Ni hapo ambapo anadaiwa kumdunga kisu msimamizi huyo wa kasino mtaa wa Eastleigh.
Kamari
Image captionMwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari
Mlinzi wa msimamizi huyo alipomkabili, naye pia akamdunga kisu na kumuua.
Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa.
Polisi wamesema mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kama John Barnabas mwenye umri wa miaka 28 anatoka eneo la Rombo, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Alikuwa akifanya kazi kama fundi wa viatu kabla ya kuanza biashara ya uchukuzi wa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya.
Kabla ya kisa hicho, waliokuwa wakifanya kazi naye wanasema alikuwa ameuza pikipiki hiyo ili kupata pesa za kwenda kucheza kamari.

exclussive,tazama video mpya ya nyimbo ya ally kiba-lupela na download hapa

Wednesday, 3 February 2016

angalia video mpya ya sean kingston-one away hapa na download bure hapa

Mwanafunzi Mtanzania avuliwa nguo hadharani huko nchini India

Gari
Image captionGari la mwanafunzi huyo Mtanzania liliteketezwa
Mwanafunzi Mtanzania alishambuliwa na kuvuliwa nguo na umati uliokuwa na hamaki katika jiji la Bangalore, kusini mwa India.
Alishambuliwa baada ya gari la mwanafunzi kutoka Sudan kumgonga na kumuua mwanamke mmoja eneo hilo.
Umati ulimvamia mwanafunzi huyo wa kike wa umri wa miaka 21 pamoja na marafiki wenzake watatu, wote kutoka Tanzania.
Walikuwa wakipitia eneo hilo muda mfupi baada ya ajali kutokea.
Umati ulimkimbiza mwanamke huyo na “kumvua blauzi”, polisi wamesema.
Ubalozi wa Tanzania umeitisha taarifa kuhusu kisa hicho, ripoti zinasema.
Kisa hicho kilitokea usiku wa Jumapili, lakini kiliripotiwa mara ya kwanza Jumanne.
Polisi wameambia mwandishi wa BBC Hindi, Imran Qureshi mjini Bangalore kwamba umati ulikusanyika eneo la Hessarghatta baada ya mwanafunzi kutoka Sudan aliyekuwa amelewa kumkanyaga mwanamke aliyekuwa amelala pembeni mwa barabara akiwa na gari lake.
Mwanafunzi huyo kutoka Sudan alipigwa na gari lake kuteketezwa lakini alifanikiwa kutoroka.
"Dakika 30 baadaye, wanafunzi wanne (kutoka Tanzania), walikuwa wakipita waliposimama na kuuliza kilichotokea. Ndipo waliposhambuliwa,” Bernandoo Kafumu, rais wa chama cha wanafunzi wa Tanzania katika chuo kimoja huko amesema.
“Mwanamke huyo hata hakumfahamu mwanamume huyo (wa Sudan) aliyehusika katika ajali hiyo,” mwanachama wa chama hicho cha wanafunzi ambaye hakutaka kutajwa amesema.
"Baada yao kushambuliwa, Watanzania hao walikimbia hadi kwenye gari lao na kujaribu kutoroka. Lakini kulikuwa na kizuizi, na walishuka na kukimbia kwa miguu. Alikimbilia maisha yake. Wenyeji walimkimbiza na kumvua nguo,” ameongeza.
Watu hao pia waliteketeza gari hilo.
Afisa wa ngazi ya juu wa polisi amethibitisha kwamba "blauzi yake iliraruliwa na kuvuliwa, lakini hakunyanyaswa kingono”.
"Baada ya habari kutokea kwenye vyombo vya habari Jumatano, tulimuomba (mwanafunzi huyo) kuwasilisha rasmi malalamishi. Tunafuata taratibu zote, atachunguzwa na daktari,” TR Suresh, naibu kamishna wa polisi wa Bangalore kaskazini, ameambia BBC Hindi.
Bangalore, ina mamia ya wanafunzi wa kigeni, wakiwemo 150 kutoka Tanzania.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...