Friday, 27 May 2016

Tazama: hawa Watu watano wafungwa maisha huko uganda.


Image captionWatu 5 waliohusika na shambulio la bomu nchin Uganda mwaka 2010 wahukumiwa maisha jela
Watu 5 waliopatikana na hatia ya mashtaka ya ugaidi kufuatia shambulio la bomu la mwaka 2010 katika mji mkuu wa Uganda Kampala ambalo liliwaua watu 74 wamepewa hukumu ya kifungo cha maisha jela.
Miongoni mwao ni Issa Ahmed Luyima ,mpangaji mkuu wa mashambulio hayo yaliodaiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi la al-Shabab.
Watu wengine wawili waliopatikana na hatia ya ugaidi walipatiwa hukumu ya kifungo cha miaka 50 jela.
Akitoa hukumu hiyo,jaji Alfonse Owiny-Dollo alisema hakuamini kwamba hukumu ya kifo itazuia visa kama hivyo.
Image captionKiongozi wa shambulio hilo Issa Ahmed Luyima
Kupatikana kwao na hatia ni mara ya kwanza kwa washukiwa wa kundi la wapiganaji wa al-Shabab nje ya Somalia.
Watu wengine sita ambao pia walishtakiwa waliachiliwa kwa mashtaka ya ugaidi na mauaji ,lakini mmoja wao alipatikana na hatia ya shtaka la kiwango cha chini.

Monday, 23 May 2016

EXCLUSIVE: baada ya van Gaal kutimuliwa MAN U Huyu hapa kocha mpya.


Image copyrightEPA
Image captionLouis Van Gaal
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi.Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.

soma hii: Milipuko mikubwa yauwa watu wengi huko Syria hivi leo



Image copyrightAFP
Image captionAssad
Takriban watu 65 wamefariki katika milipuko ya mabomu kadhaa katika maeneo muhimu ya pwani yanayodhibitiwa na serikali ya Syria ,ripoti zinasema.
Milipuko ilikumba miji ya Tartus na Jableh.
Milipuko kadhaa ilisababishwa na walipuaji wa kujitolea muhanga,kundi moja la uchunguzi limesema.
Vyombo vya habari vya Syria vinasema kuwa vituo vya mabasi ni miongoni mwa maeneo yaliolengwa .
Image copyrightREUTERS
Image captionNgome za Assad zalipuliwa
Hospitali moja pia inadaiwa kushambuliwa.
Mashambulio kama hayo si kawaida katika eneo hilo.Hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza milipuko hiyo.

Saturday, 21 May 2016

Video 10 kali kwa East Africa zilizotajwa na kituo cha TV cha Sound City cha Nigeria, watanzania 6


Jumamosi ya May 21 2016 stori ambayo imegonga headlines za muziki wa Bongo fleva ni kutoka Nigeria katika kituo cha TV cha Sound City, kituo ambacho ni moja kati ya vituo vinavyocheza video zenye viwango vya kimataifa, Sound City weekend hii imecheza TOP 10 ya video kali East Africa, kwa upande wa Tanzania wasanii sita walifanikiwa video zao kuwa katika list hiyo.View image on Twitte


10- Ben Pol – Moyo Mashine

9- Nedy Music ft Ommy Dimpoz ‘Usiende Mbali’

8- Navio – Njogereza

7- Jaguar ft Mafikizolo ‘Going Nowhere’

6- Alikiba ‘Lupela’

5- Sauti Sol ‘Unconditional Bae’

4- Vanessa Mdee ‘Niroge’

3- Kayumba ‘Katoto’

2- Eddy Kenzo ft Niniola – Mbilo Mbilo
1- G Nako ‘Original

U

video: tazama waziri Kitwanga akijibu swali akiwa amelewa bungeni na kusimamishwa kazi.

Maporomoko ya ardhi yawaua zaidi ya watu 70 na wengine 120 hawajulikani walipo.



Image captionMafuriko nchini Sri Lanka.
Utawala nchini Sri Lanka unasema kuwa zaidi ya watu 70 sasa wanafahamika kuaga dunia kwenye maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.
Zaidi ya watu wengine 120 bado hawajulikani waliko.
Katika maeneo mengine ya mji mkuu Colombo, maji yalipungua kwa kiasi leo Jumamosi lakini kwenye sehemu zingine maelfu ya watu waliolazimika kuhama kutokna na mafuriko na maporomoko ya Udongo bado wanaishi kwenye makao ya muda.
Misaada ya dharura yakiwemo mahema na mashua sasa vinawazili kutoka nchini India.

Mtu apigwa risasi kwa kubeba bunduki nje ya Ikulu


  • 21 Mei 2016
Image copyrightAP
Image captionIkulu ya White House
Afisa wa usalama wa Marekani amempiga risasi na kumjeruhi mwanamume mmoja aliyeonekana amebeba bunduki nje ya Ikulu ya White House.
Maafisa wa Usalama wamesema kuwa mtu huyo alielekea kwenye mojawapo wa milango ya kuingia katika Ikulu huku amebeba silaha hiyo. Alipoamriwa aiweke chini silaha hiyo chini akakaidi.
Image copyrightAP
Image captionWalinzi kwenye Ikulu ya White House
Watu walizuiliwa kukaribia Ikulu hiyo ya White House kwa muda, huku maafisa wa Usalama wakikimbia kuhakikisha kuwa Makamu wa Rais Joe Biden, aliyekuwa katika jengo hilo wakati huo, alikuwa salama.
Rais Obama alikuwa ameondoka kwenda kucheza mpira wa gofu.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa walisikia mlio wa risasi na kisha wakamwona mwanamume mmoja mzungu akianguka chini.

waziri afutwa kazi na rais kwa kuwa mlevi, mtazame hapa.


Image captionYaripotiwa kuwa bwana Kitwanga alienda bungeni na kujibu swali la mbunge akiwa mlevi.
Waziri wa mambo ya ndani nchini Tznania Charles Kitwanga amefutwakazi kutokana na sababu ya kuwa mlevi akiwa kazini.
Kwenye taarifa, rais John Magufuli alisema kuwa bwana Kitwanga alienda bungeni na kujibu swali la mbunge akiwa mlevi.
Hata hivyo bwana Kitwanga hajasema lolote.
Image copyrightSTATEHOUSE TANZANIA
Image captionRais John Magufuli
Rais Magufuli ambaye aliingia ofisini mwaka uliopita aliahidi kupambana na ufisadi na awewafuta kazi maafisa kadha kuhusiana na suala la ufisadi.
Lakini waandishi wa habari wanasema kuwa kufutwa kwa bwana Kitwanga ni jambo la kushangaza kwa sababu amekuwa rafiki wa rais kwa siku nyingi.

Wednesday, 18 May 2016

Soma hii: Wapiganaji wa Kiislamu wadai 'wamo Tanzania'



ISImage copyrightREUTERS
Image captionAliyesambaza video hiyo anasema wana uhusiano na Islamic State
Kundi la watu wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu limeweka video mtandaoni likidai uwepo wa wa wapiganaji wa Kiislamu nchini humo.
Video hiyo inawaonesha wanaume hao wakiwa wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga na kampeni yao.
Ukurasa wa Twitter ambao unasambaza video hiyo ya dakika tano unasema wanaume hao ni tawi la Afrika Mashariki la kundi linalojiita Islamic State (IS).
Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya usalama Afrika, Tomi Oladipo, anasema hakuna ushahidi wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya wapiganaji hao na kundi la Islamic State.
Serikali ya Tanzania imesema inafahamu uwepo wa video hiyo pamoja na ujumbe uliochapishwa kwenye Twitter na inafanya uchunguzi kubaini uhalisi wake.
Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga ameambia BBC kwa njia ya simu kwamba serikali inachukulia habari hizo kwa uzito akisema zinaweza kutishia usalama wa taifa.

Unyama: tazama video, mwanamke amkata mumewe sehemu nyeti.

HIVI PUNDE: Ndege ya Misri yapotea ikitoka Paris


  • Saa moja iliyopita
NdegeImage copyrightAFP
Image captionMwezi Machi ndege nyingine ililazimishwa kuelekea Cyprus
Ndege moja ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Maafisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikuwa na abiria 59 na wahudumu kumi.
Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya Misri.
Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga.
Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.

Tuesday, 17 May 2016

Simanzi: Wana kijiji 5 wafariki wakitafuta maji .


Image copyrightAP
Image captionUkame nchini India wasababisha uhaba wa maji
Wana kijiji watano katika eneo lililokumbwa na ukame kaskazini mwa India wamefariki wakijaribu kutafuta maji katika kisima kisichotumika.
Wanaume hao walifariki baada ya kuvuta gesi ilio na hewa chafu ambayo ilikuwa ndani ya kisima hicho katika jimbo la Haryana kulingana na afisa mmoja.
Eneo kubwa la India linakabiliwa na ukame mbaya ambao umewaua takriban watu 300.
Haryana na majimbo mengine wiki iliopita yalikosolewa na mahakama ya juu nchini India kwa kushindwa kutambua tatizo hilo la maji.
Image copyrightAFP
Image captionUhaba wa maji India
Ripoti katika eneo hilo zinasema kuwa wanaume hao kutoka wilaya ya Jindi huko Haryana waliamua kujaribu kukitengeza kisima hicho ili kuweza kukabiliana na ukosefu wa maji katika eneo hilo.
Lakini naibu afisa wa polisi katika wilya hiyo Virender Singh alikana kwamba walihitaji maji ya kunywa akisema wanaume hao walitaka kukitumia kisima hicho kwa maji ya kuoga na kuosha.
''Kisima hicho kilikuwa hakijatumika kwa takriban miaka mitano hadi sita na gesi yenye sumu ilikuwa imetanda huko chini'',aliambia kituo cha habari cha AFP.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...