Monday, 1 October 2018

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino
Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shirikisho hili litamuunga mkono rais wa sasa wa FIFA GIANNI INFANTINO katika uchaguzi wa FIFA utakaofanyika mwakani.

CAF imeweka hadharani maamuzi hayo katika mkutano wake mkuu uliofanyika nchini MISRI ambapo AHMAD amesema wao kama shirikisho na kwaniaba ya vyama vya soka vinavyounda shirikisho hilo watampigiua kura INFANTINO,

Rais wa CAF Ahmad Ahmad

Rais wa shirikisho la soka nchini MOROCCO FOUZI LEKJAA amesema mbali na kumpigia kura INFANTINO watazunguka naye sehemu yoyote dunian kama sehemu ya kampeni ili kutangaza yale mema aliyoyafanya tangu aingie madarakani.

Kwa mujibu wa tariifa mbalimbali, sera ya INFANTINO ya kuongeza nafasi za idadi ya mataifa ya afrika yatakayoshiriki katika fainali za kombe la FIFA la dunia pamoja na ahadi zinazotekelezeka ndiyo sababau kubwa iliyopekea CAF kutangaza kumuunga mkono katika uchaguzi ujao.

Rais wa FIFA Gianni Infantino
Mwezi june mwaka huu Infantino alitangaza kuwa atawania tena nafasi hiyo ya juu kabisa katika mamlaka ya soka duniani katika uchaguzi utakaofanyika mwezi JUNE mwakani jijini PARIS ingawa mpaka hivi sasa hakuna mtu aliyejitokeza kutaka kupambana naye katika nafasi hiyo ya URAIS.

TENGA apigwa chini FIFA


Rais wa chama cha soka nchini Malawi Walter Nyamilandu
Rais wa chama cha soka cha nchini MALAWI, WALTER NYAMILANDU amechaguliwa kuwa mjumbe wa baraza kuu la shirikisho la soka duniani FIFA atakayeliwakilisha shirikisho la soka barani CAF katika uchaguzi uliofanyika pale SHARM El SHEIKH nchini MISRI.

NYAMILANDU amepata kura 35 na kumshinda DANNY JORDAAN ambaye ni rais wa chama cha soka nchini AFRIKA KUSINI aliyepata kura 18 baada ya mizunguko miwili ya upigaji kura kukamilika.

Rais wa zamani wa TFF Leodgar Tenga alishindwa kwenye uchaguzi huo

Katika uchaguzi huo kulikuwa na mizunguko mitatu ya upigaji kura ambapo katika muzunguko wa kwanza walikuwepo wagombe watatu pamoja na aliyekuwa rais wa TFF LEODGAR TENGA ambaye yeye aliondolewa katika raundi hiyo ya kwanza.

Rais wa shirikisho la soka nchini KENYA, NICK MWENDWA na yule wa chama cha soka nchini SEYCHELLES, ELVIS CHETTY wenyewe walijitoa katika kinyang’anyiro hicho mapema kabla ya zoezi la upigaji kura katika mzunguko wa kwanza.

FIFA ndiyo chombo chenye maamuzi ya mwisho ya uendeshaji soka duniani

Baraza kuu la FIFA ndiyo lenye dhamana ya kuendesha na kusiamami shughuli zote za mpira wa miguu duniani na wajumbe wake hutoka katika mashirikisho ya soka kwenye mabara yote.
Uchaguzi huo umefanyika kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa rais wa chama cha soka nchini GHANA, KWESI NYANTAKYI aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa ya dola za kimarekani 65,000 kutoka kwa mwandishi wa habari aliyejifanya ni mwekezaji wa soka.

HAMILTON akaribia taji la 5 la dunia


Dereva wa kampuni ya FERARI, SEBASTIAN VERTEL anasema bado ana nafasi ya kushinda taji la mbio za langalanga msimu huu licha ya kuachwa kwa tofauti ya alama 50 na mpinzani wake mkubwa LEWIS HAMILTON. 

 HAMILTON amejiweka katika nafasi nzuri ya kushinda taji la TANO la mbio za langalanga baada ya kuibuka kinara katika michuano ya RUSSIAN GRAND PRI iliyofanyika mjini SOCHI. 

Ushindi huo unamfanya HAMILTON kufikisha alama 306 katika nafasi ya kwanza kwenye msimao huku VERTAL akiwa katika nafasi ya pili akiwa na alama 256 na VERTAL anasema anajua si kazi rahisi kupindua matokeo hayo lakini atafanya kila analoweza kuwashangaza wengi mwisho wa msimu.



Mpaka sasa yamebaki mashindano MATANO kukamilisha msimu ambayo ni pamoja na yale ya huko SUZUKA, JAPAN yatakayofanyika OCTOBA 7, mashindano ya MAREKANI yatakayofanyika OCTOBA 21mjini AUSTIN, mashindano ya MEXICO mjini MEXICO CITY, OCTOBA 28, BRAZIL mjini SAO PAULO, NOVEMBA 11 na yale yatakayofanyika mjini YAS MARINA huko ABU DHABI, NOVEMBA 25.   

Baada ya SIMBA na YANGA leo zamu ya MBAO FC

Ratiba ya mechi za ligi kuu Octoba 1

Ligi kuu TANZANIA BARA inaendelea kutimua vumbi leo jumatatu kwa michezo SITA kuchezwa katika viwanja tofauti.

Vinara wa ligi hiyo MBAO FC wenye alama 14 wanasafiri hadi kwenye dimba la MABATINI pale mlandizi-kibaha mkoani PWANI kumenyana na wenyeji RUVU SHOOTING wenye alama TANO huku maafande wa JKT TANZANIA wakiwa nyumbani kwenye dimba la JENERALI ISAMUHYO kuwaalika AFRICAN LYON.


Michezo mingine chama la wana STAND UNITED watakuwa nyumbani kwenye dimba la KAMBARAGE mjini SHINYANGA kukipiga na MBEYA CITY wakati wakulima wa alizeti SINGIDA UNITED wakiwa kwenye dimba la NAMFUA mjini SINGIDA kuwaalika wanapaluhengo LIPULI FC ya IRINGA.

Wagosi wa kaya COASTAL UNION wenyewe wana kibarua cha kukabiliana na MWADUI FC mchezo utakaopigwa kwenye dimba la MKWAKWANI jijini TANGA wakati wana tamtam MTIBWA SUGAR wakiwa katikati ya mashamba ya miwa huko TURIANI, MVOMERO mkoani MOROGORO watawakaribisha BIASHARA UNITED ya MARA kwenye dimba la MANUNGU COMPLEX. 

Watani wa jadi SIMBA na YANGA wameshindwa kutambiana 


Katika mchezo pekee wa ligi hiyo uliochezwa jana kwenye dimba la taifa jijin DSM watani wa jadi SIMBA na YANGA wameshindwa kutambiana kwa kugawana baada ya kutoka suluhu katika mchezo ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliawa na SIMBA walioshindwa kuzitumia nafasi walizopata kufunga huku mlinda mlango wa YANGA, BENO KAKOLANYA akiibuka shujaa wa mchezo huo. 

Thursday, 27 September 2018

EURO 2024 kuchezwa UJERUMANI

Hii ni mara ya kwanza Ujerumani kuandaa michuano ya Euro tangu mwaka 1988
UJERUMANI imeteuliwa kuwa wenyeji wa fainali za kombe la mataifa ya ULAYA (EURO) mwaka 2024 baada ya kuishinda UTURUKI waliokuwa wakiwania nafasi hiyo pia.

Mataifa hayo mawili yaliingia katika kinyang’anyiro cha mwisho kuwania wenyeji huo kabla ya kura zilizopigwa mjini NYON nchini USWISS yalipo makao makuu ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA ambao UJERUMANI wameibuka kidedea.

Nahodha wa zamani wa Ujeruman Philip Lahm ameteuliwa kuwa balozi wa michuano hiyo

Wenyeji huo unamaana kuwa kwa mara ya kwanza UJERUMANI itahodhi mashindano ya ulaya kama taifa MOJA baada ya iliyokuwa UJERUMANI MAGHARIBI kuandaa fainali kama hizo mwaka 1988 huku UTURUKI ikisalia bila kuandaa mashindano yoyote makubwa ya mpira katika historia yao.

Ujerumani waliomba kuanda michuano hiyo mwaka 2008, 2012, 2016 bila mafanikio

Kabla ya kupata wenyeji huo UJERUMANI iliwahi kuomba kuandaa faionali za EURO mwaka 2008, 2012 na 2016 ambako zote hawakufanikiwa lakini pia waliomba kuandaa michuano ya OLYMPIC ya mwaka 2020 ambayo nayo hawakufanikiwa baada ya kuzidiwa na JAPAN na walifanikiwa kuwa wenyeji wa fainali za kombe la FIFA la duinia za mwaka 2006.

VAR kutumika ligi ya mabingwa ulaya


Shirikisho lao soka barani Ulaya (UEFA) limesema litaanza kutumia Maamuzi ya msaada wa video (VAR) kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye msimu wa 2019-2020.

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema shirikisho lake litakuwa na mfumo ila wa kutumia VAR ili iweze kutenda haki kwa kila mtu pia watatoa mafunzo ya uhakika kwa waamuzi wote ili waweze kuelewa mfumo huo wa VAR.

Pia VAR itatumika kwenye mchezo wa Super Cup na michuano ya Ulaya ya mwaka 2020 pamoja na michuano ya Europa kwenye msimu wa 2020-2021.

VAR ilikuwa kivutio kwenye kombe la dunia huko Russia

Mfumu  wa kutumia msaada wa video  kutoa maamuzi hasa ya utata yalivutia wengi kwenye michuano ya kombe la Dunia ya mwaka huu iliyofanyika nchini Russia na ligi kubwa barani Ulaya zinatumia mfumo huo isipokuwa ligi kuu ya England.

Ronaldo kuivaa Man United

Ronaldo alioneshwa kadi nyekundu dhidi ya Valencia 

Nyota wa timu ya Juventus, Cristiano Ronaldo atacheza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya timu yake ya zamani ya Manchester United baada ya shirikikisho la soka barani Ulaya kumpa adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

Cristiano Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Valencia ya Hispania ambapo Juventus ilishinda kwa bao mbili kwa bila.

Ronaldo atacheza dhidi ya Man Utd baada ya adhabu kupunguzwa

Hiyo ilikuwa kadi nyekundi ya kwanza kwa Ronaldo kwenye michuano hiyo ya Ulaya na kama angeongezewa adhabu na UEFA basi angekosa michezo yote miwili dhidi ya Manchester United.

Kwa maamuzi hayo ya UEFA sasa Ronaldo atakosa mchezo mmoja tu dhidi ya Young Boys ya Uswiss utakaocheza Octoba pili.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...