Ninao watu wangu ambao wamefanikiwa kumaliza vyuo tena vya elimu ya juu lakini wengi wamekua wakifikiria zaidi kuajiriwa baada ya kumaliza elimu yao hiyo ya juu. Good news ambayo nakupatia ni kuwa mtu wetu Antony Luvanda ameamua kuwakutanisha wanavyuo wote kwa ajili ya kuelekezana namna unavyoweza kuitumia elimu yako bila kuajiriwa. Nimeambiwa kuwa isue hii itakua Jumamosi ya tarehe 30 pale kwenye ukumbi wa Chuo cha Duce karibu na Uwanja wa Taifa na kizuri ambacho nimeambiwa hakuna kiingilio.
anafanya maajabu katika ulimwengu wa mziki wa afrika , mpende mchukie huyu jamaa anaifanya tanzania kua nchi nyingine kabisa kisanaa.
Hii ni kolabo nyingine kutoka kwa Mtanzania Diamond Platnumz ambae zamu hii kamshirikisha mkali kutoka NigeriaMr.Flavour kwenye single inaitwa Nana kupitia kwenye mikono ya director GodFather.
Diamond Platnumz ametumia dakika hizi tatu kumwimbia mrembo aliye mbele ya macho yake,unaweza kumuandikia chochote hapa Diamond baada ya kuitazama video na atapita kusoma comments za watu wake.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye
Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW
Habari | 30.05.2015 |
Idadi ya watu waliokufa kutokana na joto kali linaloendelea
kuikumba India imepindukia 2000 leo, huku maafisa nchini humo wakisema
hali hiyo itaendelea kwa siku mbili zijazo. Wengi wa wahanga
wameripotiwa kutoka majimbo ya kusini ya Andhra Pradesh na Telangana,
ambayo wiki iliopita yameshuhudia viwango vya juu kabisa vya joto kuwahi
kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 12. Maafisa wa idara ya majanga
wamesema zaidi ya watu 200 wamefariki tangu jana mchana, na kufanya
idadi jumla ya vifo katika majimbo yote kuwa 1,979. Watu wengine 62
wameripotiwa kufariki katika majimbo ya Orissa, Mandhya Pradesh na
Gujarat, na pia katika mji mkuu wa New Delhi. Viwango vya joto katika
maeneo mengi vilikuwa kati ya nyuzi joto 40 na 45 za Celsius.
unachokiona hapo ni uwanja wa mpira wa miguu ambao unajengwa ndani ya bahari . tusubiri tuonee utakuaje baada ya kumalizika ila muonekano ndio huo hapo.
Dubaini
moja kati ya miji inayokua kwa kasi sana duniani. Na ni miongoni mwa
miji ambayo inafahamika kwa majengo ya kipekee na kifahari huku watu
wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani wakivutiwa kwenda Dubaikutalii ama kufanya biashara.
Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa mji wa Tokyo Japan muda mchache uliopita
Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa mji wa Tokyo Japan muda mchache uliopita
Tetemeko
hilo ambalo linakisiwa kuwa limefikia kipimo cha 7.8 kwenye vipimo vya
Ritcher limetokea takriban kilomita 874 kutoka Tokyo kusini mwa Japan.
Kulingana na idara ya uchunguzi wa ardhi tetemeko hili lilitokea saa tano u nusu na lilidumu kwa takriban dakika moja.
Majengo mengi yalitikiswa mjini Tokyo.
Hata hivyo hakuna taarifa zozote za uharibifu wala maafa kufikia sasa.
Tutakujuza zaidi kadri tutakavyopata habari zaidi.
Muungano wa waasi wa Syria wenye mafungamano na mtandao wa
kigaidi wa al-Qaida, umeuteka mji wa Ariha, ambao ulikuwa wa mwisho
unaoshikiliwa na serikali ya nchi hiyo katika mkoa wa Idlib.
Shirika la kuchunguza haki za binaadamu la Syria lenye makao yake
nchini Uingereza, limesema muungano huo, Al-Nusra Front na washirika
wake wa Jaish al-Fatah, au Jeshi la Ushindi, walichukua udhibiti wa mji
huo baada ya mapambano makali baina yao na jeshi la serikali ya Syria,
ambalo lilikuwa likisaidiwa na wanamgambo wa Hezbollah kutoka Lebanon.
Kundi la Al-Nusra Front limethibitisha kuuteka mji huo kupitia
mtandao wa kijamii wa Twitter, na Shirika la kuchunguza haki za
binaadamu nchini Syria limesema msafara wa magari ya kijeshi ulionekana
ukiukimbia mji huo wa Ariha.
Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari anaapishwa leo kama rais mpya wa nchi hiyo.
Bwana
Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi anachukua uongozi kutoka
kwa rais wa zamani Goodluck Jonathan ambaye amemtaka kuiunganisha nchi
hiyo wakati inapokabiliana na tisho kutoka kundi la Boko Haram.
Buhari
anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi
katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barabi afrika.
Lakini je Buhari ni nani ?
Wafuasi wa rais Buhari wakishangilia ushindi huo
Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na
aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya
mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa
Mfuko wa Amana ya Mafuta.
Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.
Buhari alimshinda rais anayeondoka Goodluck Jonathan katika uchaguzi ulioshuhudia ushindani mkubwa
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
Mkristo,
anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili,
katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.
Kuambatana
na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na
tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.
Basi
moja la uchukuzi limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na
waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre
Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
Maandamano mjini Bujumbura
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Ismael Misigaro amesema milio ya risasi inasikika mjini humo.
Maandamano
haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi
Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha
wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali
rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Mzozo huo unafuatia hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Uamuzi
ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio
iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki
kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewafuta kazi mawaziri watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu kufuatia jaribio la mapinduzi, juma lililopita.
Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi za kigeni na biashara.
Mapema hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.
Kundi la Dola la Kiislamu limetangaza limeudhibiti kikamilifu mji wa Ramadi wakati wanajeshi wa Iraq wakiripotiwa kuukimbia mji huo mkuu wa mkoa wa Anbar. Marekani inasita kuthibitisha kutekwa kwa mji huo.
Wanajeshi wa Iraq walionekana wakiukimbia mji wa Ramadi wakiziacha silaha zao na magari yasiyoweza kutobolewa na risasi, katika kile kinachoonekana kuwa pigo kubwa la kushindwa vita dhidi ya Dola la Kiislamu licha ya ongezeko la mashambulizi ya kutokea angani dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu.
Maiti zilionekana zimezagaa katika barabara za mji huo, baadhi zikiwa zimechomwa moto, huku maafisa wakiripoti kwamba wanamgambo wa kundi hilo walifanya mauaji ya kiholela ya wanajeshi wa Iraq na raia.
"Mji wa Ramadi umeanguka. Mji umedhibitiwa kabisa na jeshi linakimbia," alisema Muhannad Haimour, msemaji wa gavana wa mkoa wa Anbar.
"Tunakaribisha kundi lolote wakiwemo waasi wa kishia, waje watusaidie kuukomboa mji wetu kutoka mikononi mwa wanamgambo. Kilichotokea leo ni hasara kubwa iliyosababishwa na jeshi kushindwa kujipanga vizuri," alisema Naeem al Gououd, kiongozi wa ukoo wa madhehebu ya Sunni wakati alipozungumza na shirika la habari la Associated Press.
Mwanamume wa Kisunni akimsukuma mama mlemavu nje ya Baghdad
Gavana wa mkoa wa Anbar, Suhaib al Rawi, alisema anadhani harakati ya kijeshi inayofanywa na jeshi la Marekani ni hatua nzuri ya kuelekea kulishinda kundi la Dola la Kiislamu. "Operesheni yoyote ya maana inayofanywa na vikosi vya muungano dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu itakuwa na matokeo mazuri. Kundi hili halitishii tu usalama wa Iraq na Syria bali pia usalama wa ulimwengu mzima. Tunahitaji operesheni za namna hii, zinazotoa ishara kwamba muungano wa kimataifa umejizatiti kuyashinda makundi ya kigaidi yanayotishia sio tu mkoa wa Anbar, Iraq na Syria bali dunia nzima."
Wakaazi wakimbia Ramadi
Mamia ya wakazi wa Ramadi waliukimbia mji huo siku ya Jumamosi wakihofia mashambulizi ya wanamgambo wa Dola la Kiislamu lakini wakanyimwa ruhusa ya kuingia Baghdad na mikoa mingine na wanajeshi wa Iraq kwa sababu za kiusalama. Wakazi hao sasa wamekwama karibu na daraja la Bzibiz, kiasi kilometa 65 kutoka mji mkuu Baghdad na hawaruhusiwi kuvuka mto wa Euphrates kuelekea mji huo.
Um Mohammed, ambaye ni miongoni mwa wakaazi waliokwama, alisema hali ilikuwa ngumu Ramadi. "Vurugu, machafuko na hofu vimeenea katika barabara za Ramadi. Makombora na mabomu yalianguka kiholela kwa nyumba. Kuna ripoti mpya kwamba familia nyingi zimeuwawa. Wanawake walionekana wakikimbia mabarabarani."
Wakimbizi wa Iraq mkoani Anbar
Huku akikaribia kushindwa, waziri mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, aliamuru wanajeshi wasiondoke maeneo yao katika maeneo yote ya mkoa wa Anbar, akihofia wapiganaji wanaweza kuliteka eneo zima la jangwa lilishohudia mapigano makali baada ya uvamizi wa Iraq mnamo mwaka 2003 ulioongozwa na Marekani ambao ulimuangusha kiongozi wa zamani wa Iraq, hayati Saddam Hussein.
Marekani yafuatilia matukio ya Ramadi
Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imesema inaendelea kufuatilia ripoti za mapigano yanayoendelea mjini humo, huku ikikiri wanamgambo wa kundi hilo wanaonekana kuwa na nguvu zaidi katika makabiliano yanayoendelea. Msemaji wa wizara hiyo Maureen Schumann amesema ni mapema mno kutoa kauli kuthibitisha kinachoendelea Ramadi kwa sasa, lakini hata kama mji huo utaanguka mikononi mwa Dola la Kiislamu, muungano unaoongozwa na Marekani utawasaidia wanajeshi wa Iraq kuukomboa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alisema bado ana imani na vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu. Akiwa katika ziara nchini Korea Kusini, Kerry amesisitiza vita dhidi ya kundi hilo vitakuwa vigumu na virefu katika mkoa wa Anbar, ambako wanajeshi wa Iraq hawajakuwa imara.
Makundi ya waasi wa Kishia yamekusanyika mjini Ramadi mapema leo kuvisaidia vikosi vya Iraq kujaribu kuukomboa mji wa Ramadi.
Polisi wamelazimika kufyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura Burundi.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Maud Jullien amesema kuwa mamia ya waandamanaji walikuwa takriban kilomita moja kutoka kwa kasri ya rais ndipo wakavamiwa na maafisa wa usalama.
Polisi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura.
Hii ndio mara ya kwanza kwa waandamanji hao kukaribia kasri ya rais mjini Bujumbura tangu maelfu ya watu kuanza kuandamana kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania kuingoza taifa hilo kwa awamu ya tatu kinyume na mwafaka wa amani wa Arusha.
Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wanakutana hii leo mjini Dar es Salaam kujadili mbinu za kutatua mgogoro wa kisiasa ambao inalaumiwa kwa kusababisha vifo vya watu 20.
Mkutano huo utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo, kwenda Bujumbura wiki iliyopita.
Polisi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura.
Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo,kusikiliza hoja za viongozi wenzake.
Viongozi hao wanatarajiwa kumshinikiza rais Nkurunzinza kuahirisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi juni.
Mrembo Sitti Mtemvu zaidi ya wiki moja iliyopita alivileta kwa Watanzania vitu vyake vikubwa ambacho vitaendelea kumuweka kwenye headlines ikiwemo kitabu kiitwacho ‘Chozi la Sitti‘ pamoja na TV show yake ambayo itaanza kuonekana soon kwenye TV na anatarajia kionekane na kwenye DSTV pia.
Walikuwepo watu mbalimbali maarufu wa Tanzania wakiwemo viongozi wa serikali kama Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Sophia Simba na Naibu waziri Adam Malima kutoka Wizara ya Fedha ambapo Kitu kingine alichokileta Sitti ni Foundation yakeSitti Tanzania Foundation.
Kwenye mfululizo wa hizi picha pia kuna picha ya gari alilozawadiwa Sitti na wazazi wake….. kwa furaha akaandika ‘Wazazi wangu wamenizawadia gari la mwaka 2015, asante kwa mama na baba‘
Ni gari ambalo badala ya namba za kawaida limeandikwa jina, utaratibu ambao unaruhusiwa sasa hivi kwa Tanzania ambapo mwanzoni wakati wanatangaza huu utaratibu walisema mwenye kutaka jina badala ya namba kwenye gari atalipia shilingi MILIONI 5 kwa miaka mitatu.
Wafanyikazi wa mashirika ya kutoa misaada wamesema kuwa tetemeko la hapo jana nchini Nepal limeathiri kwa kiasi kikubwa
juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la awali lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 8000 takriban majuma mawili yaliyopita.
Mashirika ya misaada yanasema kuwa maporomoko mapya ya ardhi sasa yemekatiza usafiri baada ya kuziba mabarabara yaliyokuwa yamesazwa na tetemeko la awali.
Hadi kufikia sasa inakisiwa kuwa takriban watu 65 wamepoteza maisha yao nchini Nepal huko maafa zaidi yakitarajiwa nchini India na Tibet ,China.
Shughuli za uokozi zimerejelewa Nepal, ambayo kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu imekumbwa na tetemeko kubwa la ardhi.
Wahathiriwa wengi wameripotiwa kufunikwa na vifusi karibu na kitovu cha tetemeko hilo katika mji wa Chautara
Lakini bado kuna watu waliozikwa kwenye vifusi.
Maafisa wa huko wanasema kuwa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.
Kufikia sasa takriban watu 1,000 wamejeruhiwa na tetemeko hilo lipya.
Waathiriwa wengi wameripotiwa kufunikwa na vifusi karibu na kitovu cha tetemeko hilo katika mji wa Chautara
Watu wengi wamelala nje wakihofia kuwa wanaweza kuathirika zaidi wakiwa ndani ya nyumba zao.
Hadi kufikia sasa inakisiwa kuwa takriban watu 65 wamepoteza maisha yao
Wakati huo huo helikopta ya kikosi cha majini cha Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani iliko.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya helikopta hiyo kulikuwa na watu wanane,miongoni mwao, sita ni askari wa kikosi cha majini cha Marekani na askari wawili wa jeshi la Nepal.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helikopta hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.